TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 05 Agosti, 2020 amewasili Dodoma akitokea Jijini Dar es Salaam.

Akiwa njiani, Mhe. Rais Magufuli amewasalimu wananchi wa Dumila katika Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro ambao wanajishughulisha na biashara ndogondogo za kuuza mahindi ya kuchoma, mahindi mabichi, Nyanya, Vitunguu, mbogamboga na bidhaa nyingine zinazozalishwa katika eneo hilo.

Mhe. Rais Magufuli amekubali ombi la wananchi hao la kupanuliwa kwa barabara na kujengwa kwa vibanda vya biashara katika eneo hilo, kwa kuwa mazingira yaliyopo sasa ni finyu na hatarishi kutokana na kusongamana katika barabara kuu.

Mhe. Rais Magufuli ameahidi kuwa Serikali itatoa shilingi Milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa vibanda hivyo na pia amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) katika Mkoa wa Morogoro kufanya upanuzi wa barabara katika eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *