Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan Azungumza na Viongozi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini Mkoani Dar es Salaam tarehe 25 Juni, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya ambaye ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Gervas Nyaisonga mara baada ya kuwasili katika Makao Makuu (TEC) Kurasini mkoani Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Jude Thaddeus Ruwa’ichi mara baada ya kuwasili katika Makao Makuu ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Kurasini mkoani Dar es Salaam leo tarehe 25 Juni, 2021. Katikati ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mbeya ambaye pia ni Rais wa TEC Askofu Gervas Nyaisonga na wakwanza kulia ni Askofu Augustine Shao kutoka Jimbo Katoliki Zanzibar
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania TEC katika ukumbi wa AMECEA Kurasini mkoani Dar es Salaam.
Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini wakiwa wamesimama kushukuru mara baada ya hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Makao Makuu ya TEC Kurasini Mkoani Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiagana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mbeya ambaye pia ni Rais wa TEC Askofu Gervas Nyaisonga mara baada ya kupiga picha za kumbukumbu na Maaskofu wa TEC Kurasini mkoani Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *