Matukio Mbalimbali ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Akihitimisha Ziara yake Nchini Burundi tarehe 17 Julai, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye wakipokea heshima ya wimbo wa Taifa walipowasili  katika Ukumbi wa Royal Jijini Bujumbura kwa ajili ya kuhutubia katika Jukwa la Wafanyabiashara wa Tanzania na Burundi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye wakiangalia moja ya ngoma ya asili ya Burundi walipowasili katika Ukumbi wa Royal Jijini Bujumbura kwa ajili ya kushiriki katika Jukwa la Wafanyabiashara wa Tanzania na Burundi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye mkutano wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Tanzania na Burundi Bujumbura Nchini Burundi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Watanzania wanaoishi nchini Burundi alipokutana nao Jijini Bujumbura Nchini Burundi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Viongozi mbalimali wa Serikali ya Burundi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Melchior Ndadaye  Jijini Bujumbura Burundi baada ya kukamilisha ziara yake ya Kitaifa ya siku mbili Nchini Burundi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Rais wa Jamhuri ya Burundi  Mhe. Evariste Ndayishimiye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Melchior Ndadaye  Jijini Bujumbura Burundi baada ya kukamilisha ziara yake ya Kitaifa ya siku mbili Nchini Burundi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *