MATUKIO MBALIMBALI YA ZIARA YA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN NCHINI RWANDA TAREHE 02-03 AGOSTI, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipowasili Uwanja wa ndege wa Kigali nchini rwanda na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje ya Rwanda, Mhe. Vicent Biruta.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride alipowasili Ikulu ya Kigali, nchini rwanda tarehe 02 Agosti, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokelewa na mwenyeji wake Mhe. Paul Kagame mara baada ya kuwasili Ikulu ya Kigali nchini Rwanda, tarehe 02 Agosti, 2021.
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais Paul kagame wa Rwanda wakati wakielekea katika chakula cha jioni alichondaliwa na mwenyeji wake nchini humo.
Mhe. Rais Samia akihutubia wakati wa dhifa iliyoandaliwa tarehe 02 Agosti, 2021.
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akiweka saini kitabu cha kumbukumbu alipotembelea Makumbusho ya Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda.
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua katika makaburi yaliyopo katika Makumbusho ya Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda tarehe 02 Agosti, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana  na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame mara baada ya kuwasili katika eneo la Uwekezaji wa kiwanda cha Inyange Plant Entrance kilichopo mjini Kigali Rwanda tarehe 03 Agosti, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na mwenyeji wake Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakiangalia baadhi ya Bidhaa mbalimbali zinazozalishwa katika kiwanda cha Inyange Plant mjini Kigali wakati walipotembelea kiwanda hicho tarehe  03 Agosti, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia moja ya aina ya simu zinazotengenezwa katika kiwanda cha Mara Phone Mjini Kigali Rwanda, wakati alipokua katika ziara yake ya siku ya pili nchini Rwanda tarehe 03 Agosti, 2021. Kulia ni Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakiwa mbele ya Gari aina ya Volkswagen mara baada ya kutembelea kwenye Kiwanda cha kutengenezea Magari CFAO MOTORS Mjini Kigali Nchini Rwanda leo tarehe  03 Agosti, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Rwanda baada ya kukamilisha ziara yake ya siku mbili Nchini Rwanda tarehe  03 Agosti, 2021.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *