Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Asimikwa Rasmi kuwa Mkuu wa Machifu Tanzania katika Tamasha la Utamaduni (Mila na Desturi zetu) tarehe 08 Septemba, 2021 Mkoani Mwanza


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwanza tarehe 08 Septemba, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kikundi cha ngoma za asili cha Chapakazi kilichokuwa kikitumbuiza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwanza tarehe 08 Septemba, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akivalishwa Mavazi ya Kimila kuwa  Chifu Mkuu wa Machifu wote Tanzania na kuitwa jina la Hangaya yani ni Nyota inayong`aa, katika Tamasha la Utamaduni (Mila na Desturi zetu) lililofanyika katika Viwanja vya Redcross Kisesa Magu, Mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Mkuki na Ngao kutoka kwa Chifu Fundi Kira Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu Tanzania mara baada ya kusimikwa kuwa Mkuu wa Machifu wote Tanzania na kuitwa jina la Hangaya yani Nyota inayong`aa, katika Tamasha la Utamaduni (Mila na Desturi zetu) lililofanyika katika Viwanja vya Redcross Kisesa Magu, Mkoani Mwanza.
Wananchi wa Mwanza wakiwa katika Tamasha la Utamaduni (Mila na Desturi zetu) lililofanyika katika Viwanja vya Red Cross Mkoani Mwanza.
 
Machifu kutoka Mikoa mbalimbali nchini wakiwa katika Tamasha la Utamaduni (Mila na Desturi zetu) lililofanyika katika Viwanja vya Red Cross, Magu Mkoani Mwanza .
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma akitokea  Jijini Mwanza baada ya kusimikwa kuwa Mkuu wa Machifu wote Tanzania na kuitwa jina la Hangaya yani ni Nyota inayong’aa, katika Tamasha la Utamaduni (Mila na Desturi zetu) lililofanyika lViwanja vya Redcross Kisesa Magu, Mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Serikali alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma akitokea  Jijini Mwanza baada ya kusimikwa kuwa Mkuu wa Machifu wote Tanzania na kuitwa jina la Hangaya yani ni Nyota inayong’aa, katika Tamasha la Utamaduni (Mila na Desturi zetu) lililofanyika lkatika Viwanja vya Redcross Kisesa Magu, Mkoani Mwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *