TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wafuatao:-

  1. Amemteua Dkt. Yamungu Kayandabila kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).

Dkt. Kayandabila ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  1. Mhe. Rais Samia amemteua Dkt. Naomi Bakunzi Katunzi kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa kipindi kingine cha miaka mitatu (3).

Uteuzi huu umeanza tarehe 14 Septemba, 2021.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *