Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Ahutubia Mkutano wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Kuongoza kuaga mwili wa Marehemu Ole Nasha Jijini Dodoma tarehe 30 Septemba, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Hayati William Tate Ole Nasha katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisaini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo  kufuatia kifo cha aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Hayati William Tate Ole Nasha wakati wa kuaga mwili wa Naibu Waziri huyo katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima akimkabidhi Tuzo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kutambua kazi kubwa anayoifanya katika kujenga Taifa la Tanzania, kwenye mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini (NGO’s) uliofanyika leo Sept 30,2021 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete  Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Taarifa ya Kielektroniki ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali NGO’s kwa maendeleo ya Taifa katika mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini (NGO’s) uliofanyika Sept 30, 2021 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete  Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akionesha Taarifa ya Kielektroniki ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali NGO’s kwa maendeleo ya Taifa katika mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini (NGO’s) uliofanyika Sept 30, 2021 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete  Jijini Dodoma.
.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kuhusu utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kazi za Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini (NGO’s) alipotembelea mabanda ya maonesho katika mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini (NGO’s) uliofanyika Sept 30, 2021 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete  Jijini Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *