Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na Rais Yoweri Museveni wa Uganda Washiriki katika Uzinduzi wa Shule ya Awali na Msingi Museveni yenye Mtaala wa Kingereza Chato mkoani Geita leo tarehe 29 Novemba, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kwa pamoja wakiondoa kitambaa  kuzindua rasmi Shule ya Awali na Msingi Museveni Pre & Primary School  iliyojengwa kwa msaada wa Rais  Yoweri Museveni Wilayani Chato Mkoani Geita leo tarehe 29 Novemba 2021.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kwa pamoja wakikata utepe kuzindua rasmi Shule ya Awali na Msingi Museveni  iliyojengwa kwa msaada wa Rais  Yoweri Museveni Wilayani Chato Mkoani Geita leo tarehe 29 Novemba 2021.
Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akimkabidhi mfano wa funguo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kama ishara ya makabidhiano ya Shule hiyo ya Awali mara baada ya uzinduzi uliofanyika katika Shule hiyo ya Museveni  Chato mkoani Geita leo tarehe 29 Novemba 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakikagua baadhi ya majengo ya Shule hiyo ya Awali na Msingi iliyojengwa kwa msaada wa  Rais Yoweri Museveni Chato mkoani Geita leo tarehe 29 Novemba 2021 mara baada ya kuizindua rasmi Shule hiyo.
 
.
.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda katika Uwanja wa ndege wa Chato Mkoani Geita, baada ya Rais Museven kukamilisha ziara yake ya Kitaifa ya Kiserikali hapa Nchini leo tarehe 29 Novemba 2021.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *