Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan aendelea na Ziara yake ya kikazi Nchini Ufaransa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishuhudia utiaji saini wa mikataba ya ushirikiano katika sekta mbalimbali kati ya Tanzania na Ufaransa  iliyosainiwa  na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula pamoja na Waziri wa Biashara wa Ufaransa Frank Reicster katika mji wa Brest nchini Ufaransa tarehe 11 Februari, 2022
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Biashara wa Ufaransa Frank Reicster kabla ya kushuhudia utiaji saini wa mikataba ya ushirikiano katika sekta mbalimbali katika Tanzania na Ufaransa katika mji wa Brest nchini Ufaransa tarehe 11 Februari, 2022
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akioneshwa kazi mbalimbali za ujenzi wa vyombo vya usafiri wa majini ikiwemo boti za uokoaji na doria katika mji wa Brest nchini Ufaransa leo tarehe 11 Februari, 2022
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwigulu Nchemba akiweka saini moja ya mikataba ya ushirikiano wa kimaendeleo katika Nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Ufaransa iliyowakilishwa na Waziri wake wa Biashara Frank Reicster katika mji wa Brest nchini Ufaransa tarehe 11 Februari, 2022.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *