MABADILIKO MADOGO YA MAKATIBU WAKUU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Makatibu Wakuu kama ifuatavyo:
- Dkt. Francis Michael, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anahamishiwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
- Prof. Eliamani Sedoyeka, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anahamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Viongozi hao wataapishwa katika tarehe itakayotangazwa baadae.