Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Azindua Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation, Zanzibar Tarehe 20 Juni, 2022

.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akisalimiana na Viongozi, Wanafunzi na Wananchi alipowasili katika ukumbi wa Golden Tulip, Zanzibar tarehe 19 Juni, 2022 kwa ajili ya kuzinduzia Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) katika hafla iliyofanyika kwenye Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar tarehe 19 Juni, 2022. Taasisi hiyo iliyozinduliwa ina lengo la kumsaidia mtoto wa Kike Shuleni pamoja na Watoto wengine ili kuhakikisha wanatimiza ndoto zao kielimu na kimaisha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali kabla ya kuzindua Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) katika hafla iliyofanyika kwenye Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar tarehe 19 Juni, 2022.
Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) Mhe. Wanu Hafidh Ameir akizungumza na Viongozi mbalimbali kabla ya uzinduzi wa Taasisi hiyo uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar tarehe 19 Juni, 2022.
Viongozi pamoja na Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) uliofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar tarehe 19 Juni, 2022.
.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo yenye saini 50 za Wanafunzi Wanawake waliofaidika na Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) katika hafla iliyofanyika kwenye hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar tarehe 19 Juni, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein mara baada ya uzinduzi wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) uliofanyika kwenye Hotel ya Golden Tulip, Zanzibar tarehe 19 Juni, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Viongozi na Wananchi baada ya kuzindua rasmi Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) katika hafla iliyofanyika kwenye Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar tarehe 19 Juni, 2022.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *