TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 04 Julai, 2022 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, (TPA) Ndugu Eric Hamissi.

Ndugu Plasduce Mkeli Mbossa anachukua nafasi ya Ndugu Eric Hamissi ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Kabla ya uteuzi huo Ndugu Mbossa alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania.

Uteuzi huu umeanza tarehe 04 Julai, 2022.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *