Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa Wapya 09, kuwahamisha vituo vya kazi Wakuu wa Mikoa 07 na wengine 10 kubakia kwenye vituo vyao kama ifuatavyo:
- WAKUU WA MIKOA WAPYA:
- Nurdin Hassan Babu – Ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido mkoani Arusha.
- Fatma Abubakar Mwasa – Ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
- Halima Omari Dendego – Ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
- Dkt. Raphael Masunga Chegeni – Ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
- Peter Joseph Serukamba – Ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
- Kanali Ahmed Abbas Ahmed – Ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara. Alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani.
- Kanali Laban Elias Thomas – Ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma. Alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.
- Albert John Chalamila – Ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera
- Dkt. Yahaya Esmail Nawanda – Ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu. Alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora mkoani Tabora.
- WALIOHAMISHWA VITUO VYA KAZI:
- Anthony John Mtaka – Amehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
- Queen Cuthbert Sendiga – Amehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
- Waziri Waziri Kindamba – Amehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
- Martin Reuben Shigella – Amehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
- Omary Tebweta Mgumba – Amehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe.
- Adam Kigoma Malima – Amehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
- Rosemary Staki Senyamule – Amehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita.
- AMBAO WANAENDELEA NA VITUO VYA KAZI:
- Amos Gabriel Makalla – Anaendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
- John Vianney Mongella – Anaendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
- Mwanamvua Hoza Mrindoko – Anaendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
- Charles Makongoro Nyerere – Anaendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
- Zainab Rajab Telack – Anaendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
- Juma Zuberi Homera – Anaendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
- Thobias Emir Andengenye – Anaendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
- Sophia Edward Mjema – Anaendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
- Balozi Batilda Salha Burian – Anaendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
- Abubakar Mussa Kunenge – Anaendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Uapisho utafanyika Ikulu Chamwino, Dodoma tarehe 1, Agosti, 2022.