RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AIFARIJI FAMILIA YA NYERERE KUFUATIA KIFO CHA JOHN NYERERE MEI 12, 2015

1

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo Mei 12,2015  nyumbani kwa Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mwanaye John Nyerere kilichotokea hivi karibuni.Aliyesimama pembeni ya Rais ni mdogo wa marehemu Makongoro Nyerere.

2

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya marehemu John Nyerere nyumbani kwao Msasani jijini Dar es Salaam leo asubuhi.  3

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mwanaye John Nyerere kilichotokea juzi .Mwili wa Marehemu John Nyerere rubani wa zamani wa ndege za kivita nchini aliyeshiriki kikamilifu vita vya Uganda kati ya mwaka 1978 na 1979, unatarajiwa kusafirishwa Mei 12,2015  kwenda kijijini Butiama mkoani Mara kwa maziko

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *