RAIS WA INDIA NA WAZIRI MKUU WA INDIA WAMPOKEA RASMI RAIS KIKWETE IKULU YA INDIA JUNI 19,2015

unnamedRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Waziri Mkuu wa India, Mheshimiwa Narendra Modi mara baada ya kuwasili Ikulu ya India kwa sherehe za ukaribisho wake rasmi nchini India kwa ajili ya ziara yake ya Kiserikali. Sherehe hizo zimefanyika asubuhi ya Juni 19, 2015.

unnamed-1Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, Waziri Mkuu wa IndiaMheshimiwa Narendra Modi, na Rais Wa IndiaMheshimiwa Pranad Mukherjee wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya Rais kikwete kuwasili katika ikulu ya India kwa mapokezi rasmi

unnamed-2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la Majeshi ya India liliandaliwa kwa ajili ya kumkaribisha kwa ziara rasmi ya Kiserikali nchini India katika sherehe za ukaribisho zilizofanyika asubuhi ya  Juni 19, 2015.

unnamed-3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Rais wa India, Mheshimiwa Pranad Mukherjee (kushoto) na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Narendra Modi mara baada ya kumalizika kwa sherehe za kumkaribisha nchini India kwa ziara rasmi ya Kiserikali. Sherehe hizo zimefanyika Ikulu ya India mjini New Delhi, asubuhi ya  Juni 19, 2015.

unnamed-4

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakiweka shada katika kaburi la mpigania uhuru na muasisi wa taifa la India Mahatma Ghandi jijini New Delhi India Juni 19,2015

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *