RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AFUNGUA MAJENGO YA TAASISI ZA FEDHA DODOMA OKTOBA 15, 2015

1

 

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Benno Ndulu akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete albam ya picha mbalimbali za Rais zinazohusiana na shughuli za Benki kuu wakati hafla ya uzinduzi wa Jengo la Tawi la Benki kuu mjini Dodoma leo.Kulia ni Waziri wa Fedha Saada Mkuya.

2

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Fedha Bibi Saada Mkuya na Gavana wa Benki Kuu Professa Benno Ndulu wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa waandamizi wa benki kuu pamoja na wafanyakazi wa Benki kuu Tawi jipya la Dodoma muda mfupi baada ya hafla wa uzinduzi wa tawi hilo. 

13

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni mashuhuri wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo la Tawi jipya la Benki Kuu mjini Dodoma leo huku Waziri wa Fedha Bibi Saada Mkuya na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu wakishuhudia.

12

 

11 Baadhi ya Watumishi kutoka Benki Kuu,Hazina na Ofisi ya Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali wakisikiliza hotuba ya Rais Kikwete muda mfupi baada ya kufungua majengo matatu ya taasisi hizo mjini Dodoma

10

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni mashuhuri wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo la Tawi jipya la Benki Kuu mjini Dodoma leo huku Waziri wa Fedha Bibi Saada Mkuya na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu wakishuhudia.

9

 

8

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Fedha Bibi Saada Mkuya(Wanne kushoto),Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Professa Mussa Assad(wapili kushoto), Katibu Mkuu Hazina Dkt.Servacius Likwelile(kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali iliyofunguliwa rasmi mjini Dodoma 

7

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Professa Musa Assad akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitabu kinachohusu kanuni na utendaji wa kazi za ofisi yake wakati wa uzinduzi wa jengo la ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali uliofanyika mjini Dodoma 6 

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Fedha bibi Saada Mkuya, Mdhibiti  na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali Professa Musa Assad na Katibu Mkuu Hazina Dkt. Servacious Likwelile wakikata utepe kufungua jengo la ofisi za CAG mjini Dodoma

5

 

4

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kufungua rasmi jengo la Wizara ya Fedha mjini Dodoma leo.Kulia ni Waziri wa Fedha Bibi Saada Mkuya.

3Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni mashuhuri wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo la Tawi jipya la Benki Kuu mjini Dodoma leo huku Waziri wa Fedha Bibi Saada Mkuya na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu wakishuhudia