Author Archives: Sharifa Nyanga

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Prof. Mark James Mwandosya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).  Prof. Mwandosya anachukua nafasi ya Prof. Jamidu Hazzam Yahaya ambaye amemalizia muda wake.

Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Agosti, 2022.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan aanza ziara ya siku moja nchini Congo DRC tarehe 18 Agosti, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo wakipokea Gwaride rasmi alipowasili katika Viwanja vya Ikulu Jijini Kinshasa kwa ajili ya kuanza ziara rasmi ya siku moja nchini DRC tarehe 18 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo akikagua Gwaride rasmi alipowasili katika Viwanja vya Ikulu Jijini Kinshasa kwa ajili ya kuanza ziara rasmi ya siku moja nchini DRC tarehe 18 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo alipokua akitambulishwa kwa Viongozi mbalimbali wa DRC alipowasili katika Ikulu ya Kinshasa kwa ajili ya kuanza ziara rasmi ya siku moja tarehe 18 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo katika Ikulu ya Kinshasa nchini DRC tarehe 18 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo alipowasili katika Viwanja vya Ikulu ya Kinshasa tarehe 18 Agosti, 2022