RAIS DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA AUSTRALIA NA GAVANA MKUU WA NCHI HIYO 28 JULAI 2015

1

 

2wewwe Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot alipowasili asubuhi ya tarehe  28 Julai 2015  katika makao  Makuu ya kiongozi  huyo  jijini Sydney 

3Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo rasmi na Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot asubuhi ya tarehe  28 Julai 2015 katika makao  Makuu ya kiongozi  huyo  jijini Sydney  

4Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la lililoandaliwa kwa heshima yake huku akipigiwa mizinga 21 alipowasili asubuhi ya tarehe  28 Julai 2015 katika makao  Makuu ya kiongozi  huyo  jijini Sydney

5Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiutambulisha ujumbe wake kwa Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot alipowasili asubuhi ya tarehe  28 Julai, 2015 katika makao  Makuu ya kiongozi  huyo  jijini Sydney 

6Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni alipowasili kwenye jumba la serikali jijini Sydney tarehe 28 Julai 2015 na kukutana na kufanya mazungumzo na  Gavana Mkuu wa Australia Mheshimiwa Peter Cosgrove aliyesimama nyuma yake pamoja na Mama Salma Kikwete na Mke wa Gavana huyo Mama Cosgrove.  

7Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati wa chakula cha mchana kwenye jumba la serikali jijini Sydney tarehe 28 Julai 2015 baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na  Gavana Mkuu wa Australia Mheshimiwa Peter Cosgrove.

 

 RAIS DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI MKUU WA AUSTRALIA JULAI 28,2015.

Waziri Mkuu wa Australia, Bwana Tony Abbot amempongeza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuamua kukabidhi madaraka kwa kiongozi mwingine kwa mujibu wa  Katiba nchini Tanzania.

“Nakupongeza sana kwa uamuzi wako wa kukabidhi madaraka kwa amani nchini kwako , ni jambo la nadra sana Barani Afrika, kuwa na utaratibu mzuri na wa Amani  namna hii” Bw. Abbot amemuambia Rais Kikwete na kumueleza awe  na uhakika  kuwa ” Australia itaendelea kuisaidia Tanzania katika juhudi zake za kuleta maendeleo na kukuza  uchumi” ameongeza.

Rais Kikwete na Waziri Mkuu Abbot pia wamezungumzia jinsi nchi zao zinaweza kuendelea kushirikiana katika kulinda usalama baharini, kukuza zaidi ushirikiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kijamii.

Rais Kikwete yuko nchini Australia kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa Australia Mheshimiwa Peter Cosgrove.

Rais Kikwete amepokelewa leo asubuhi tarehe  28 katika makao  Makuu ya kiongozi  wa Australia kwa heshima zote kwa kupigiwa mizinga 21 na kuandaliwa chakula rasmi cha mchana na baadae kupanda mti  kuashiria kuimarisha mashirikiano baina ya nchi hizi mbili kwa kipindi kirefu kijacho.

Tanzania na Australia zimedumu katika ushirikiano  baina ya nchi zao tangu miaka ya sitini na sasa nchi mbili hizi zimeazimia kuimarisha mahusiano haya  zaidi katika sekta mbalimbali zikiwemo za uwekezaji na biashara kati yao.

Baadae leo jioni Rais Kikwete atakutana na wawekezaji wakubwa wa Australia ambao tayari wanawekeza nchini Tanzania kwa ajili ya mazungumzo ya namna ya kuendeleza sekta mpya ya gesi nchini na jinsi Tanzania inaweza kunufaika  kutokana na kupata gesi.

Tayari Serikali ya Australia na makampuni binafsi ya gesi na mafuta, yanaisaidia Tanzania hasa katika vyuo vya ufundi stadi VETA na  tafiti mbalimbali katika Kilimo.

Kesho tarehe 29 Julai, 2015 Rais Kikwete anatarajia kutunukiwa digrii ya udaktari wa heshima ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Newcastle, kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika uongozi kwa kipindi cha miaka 10 aliyokaa madarakani nchini Tanzania na Dunia kwa ujumla.

Rais Kikwete anatarajia kuondoka Australia na kurejea Tanzania baada ya shughuli ya kupokea shahada yake na ratiba yake kwa ujumla.

Imetolewa na:

Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi

Canberra-Australia

28 Julai, 2015

 

1 thought on “RAIS DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA AUSTRALIA NA GAVANA MKUU WA NCHI HIYO 28 JULAI 2015

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *