MHE. RAIS Dkt. J.P.MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO WA MABALOZI WATEULE WA MAREKANI NA VIETNAM WATAKAO ZIWAKILISHA NCHI ZAO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Marekani hapa nchini Donald John Wright mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwake katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi katika picha ya pamoja na Balozi wa Marekani hapa nchini Donald John Wright Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi katika picha ya pamoja na Balozi wa Viet Nam hapa nchini Nguyen Nam Tien mara baada ya kuwasili

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Marekani hapa nchini Donald John Wright 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Balozi wa Viet Nam hapa nchini Nguyen Nam Tien mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwake katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

PICHA MBALIMBALI ZA MABALOZI  WALIPO WASILISHA HATI ZAO IKULU

 

HABARI PICHA MHE RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO AKIWA NJIANI KUREJEA DAR KUTOKA LUPASO MKOANI MTWARA KWENYE MAZISHI YA RAIS MSTAAFU B.W.MKAPA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Nangulukulu mkoani Lindi kuhusu ubovu wa barabara ya kutokea Lindi- Somanga wakati alipokuwa akitokea Msibani Masasi mkoani Mtwara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya Jogoo alilopewa na Mzee Shaweji Mohamed Kimbwembwe mkazi wa Somanga mkoani Lindi ambaye alifurahishwa na utendaji kazi wa Mhe. Rais Magufuli wa kuwaletea maendeleo Wananchi wanyonge.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na zawadi ya Jogoo alilopewa na Mzee Shaweji Mohamed Kimbwembwe mkazi wa Somanga mkoani Lindi ambaye alifurahishwa na utendaji kazi wa Mhe. Rais Magufuli wa kuwaletea maendeleo Wananchi wanyonge.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Somanga Rehema Mikidadi Ngenje Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya ukarabati wa Shule hiyo ya Msingi ya Somanga. Katika fedha hizo pia Rais aliagiza mwanafunzi huyo apewe Shilingi laki moja kutoka kwenye fedha hizo mara baada ya kuibua kero ya Shule hiyo

Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Somanga Rehema Mikidadi Ngenje  akiwa ameshikilia Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya ukarabati wa Shule hiyo ya Msingi ya Somanga. Katika fedha hizo pia Rais aliagiza mwanafunzi huyo apewe Shilingi laki moja kutoka kwenye fedha hizo mara baada ya kuibua kero ya Shule hiyo, kushoto ni mwalimu wa shule hiyo Mariam Bakari.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Wananchi wa Somanga mkoani Lindi mara baada ya kuwahutubia wakati akitokea Masasi mkoani Mtwara

Mzee Shaweji Mohamed Kimbwembwe mkazi wa Somanga mkoani Lindi akiliandaa Jogoo baada ya kumzawadia  Rais,  kwa kufurahishwa na utendaji kazi wa Mhe. Rais Magufuli wa kuwaletea maendeleo Wananchi wanyonge

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipita na kukagua Daraja la Mkapa linalopita katika Mto Rufiji mkoani Pwani wakati akitokea Masasi Mtwara kwenye msiba wa Marehemu Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa leo tarehe 30 Julai 2020. Daraja hilo linalounganisha Pwani na Mikoa ya Lindi na Mtwara lilijengwa na Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Marehemu Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa