Daily Archives: October 6, 2021

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Azindua Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Jijini Dodoma tarehe 06 Oktoba, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa Kitambaa kuzindua rasmi Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji  Haki katika eneo la National Capital City, Jijini Dodoma leo tarehe 06 Oktoba 2021. Wa pili kulia ni Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma, Jaji Mkuu wa Zanzibar Othman Makungu, wa pili kushoto ni Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Palamagamba Kabudi na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata Utepe kuzindua rasmi Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki katika eneo la National Capital City Jijini Dodoma leo tarehe 06 Oktoba 2021. Wa pili kulia ni Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma, Spika wa Bunge Job Ndugai, Jaji Mkuu wa Zanzibar Othman Makungu wa pili kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Palamagamba Kabudi, Mkuu wa Mkoa Dodoma Antoni Mtaka.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kuhusu sehemu ya uendeshaji Haki mara baada ya kuzindua rasmi Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji  Haki katika eneo la National Capital City Jijini Dodoma leo tarehe 06 Oktoba, 2021. Wa pili kulia ni Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma, Jaji Mkuu wa Zanzibar Othman Makungu, wa pili kushoto ni Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Palamagamba Kabudi na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai.
.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia wakati wa uzinduzi  wa Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji  Haki katika eneo la National Capital City, Jijini Dodoma leo tarehe 06 Oktoba 2021.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, tarehe 05 Oktoba, 2021 amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Uchumi Afrika (Arab Bank for Economic Development in Africa – BADEA) Dkt. Sidi Ould Tah, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Katika mazungumzo hayo, Dkt. Ould Tah amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa kuzungumza nae na kumhakikishia kuwa BADEA itaendelea kuunga mkono jitahada za Serikali ya Tanzania katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Aidha, Dkt. Ould Tah ameutambulisha mkakati mpya wa BADEA 2030 ambao unaainisha fursa zitokanazo na ongezeko la mtaji kutoka kwa wanahisa wake na kuwezesha kuongezeka kwa utoaji wa misaada na mikopo kwa mwaka.

Dkt. Ould Tah amesema mkakati huo unajikita kwenye miundombinu, vijana na wafanyabishara wadogo na wa kati, kuongeza mnyororo wa thamani katika kilimo, biashara na sekta binafsi pamoja na kuwajengea uwezo wahusika wa miradi hiyo.

Kwa upande wake Mhe. Rais Samia ameishukuru BADEA kwa kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika miradi ya maendeleo na utaalamu  kwa zaidi ya miaka 40.

Aidha, Mhe. Rais Samia ameishukuru BADEA kwa kuonyesha fursa zilizopo katika mkakati wao mpya unaoendana na Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP III), unaolenga kuongeza ufanisi na ushindani  kwa kuimarisha miundombinu, biashara, sekta binafsi pamoja na  kuwajengea uwezo vijana na wafanyabishara wadogo na wa kati.