Daily Archives: October 10, 2021

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wafuatao:-

  1. Amemteua Mhe. Sofia Edward Mjema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Mhe. Mjema anachukua nafasi ya Dkt. Philemon Sengati, ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Kabla ya uteuzi huo, Mhe. Mjema alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

  • Amemteua Mhe. Jaji Omar Othman Makungu kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania.

Kabla ya uteuzi huo, Jaji Makungu alikuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar.

  • Amemteua Mhe. Jaji Mustapha Siyani kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Kabla ya uteuzi huo Jaji Siyani alikuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Jaji Eliezer Felishi aliyeteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Uteuzi huu umeanza tarehe 07 Oktoba, 2021. Wateule hao wataapishwa tarehe 11 Oktoba, 2021 saa 05:00 Asubuhi, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.