Daily Archives: October 21, 2021

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemteua Prof. Penina Oniviel Muhando kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).

Prof. Muhando anachukua nafasi ya Prof. Mayunga Habibu Hemedi Nkunya ambaye alifariki tarehe 20 Julai, 2021.

Uteuzi huo umeanza tarehe 19 Oktoba, 2021.