Daily Archives: November 10, 2021

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Aelekea Nchini Misri kwa Ziara ya Siku 3 tarehe 10 Novemba, 2021


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono viongozi mbalimbali waliomsindikiza katika uwanja wa Ndege wa Dodoma wakati akielekea Cairo nchini Misri kwa ajili ya Ziara ya Kiserikali ya siku tatu.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango katika uwanja wa Ndege wa Dodoma kabla ya kuondoka nchini kuelekea Cairo, Misri kwa ajili ya Ziara ya Kiserikali ya siku tatu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango wakati akielekea kupanda Ndege kwenda Cairo, Misri kwa ajili ya Ziara ya Kiserikali ya siku tatu

UTEUZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemteua Prof. Wineaster Saria Anderson kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE).

Prof. Anderson anachukua nafasi ya Prof. Eleuther Mwageni ambaye alifariki mwezi Julai, 2021.

Uteuzi huo umeanza tarehe 07 Novemba, 2021.