Monthly Archives: December 2021

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali: –

  1. Amemteua Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Chancellor) kwa kipindi kingine cha miaka sita (06) kuanzia tarehe 17 Januari, 2022.
  • Amemteua Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia (CFR). Balozi Mwinyi ni Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
  • Amemteua Balozi Begium Kaim Taji kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Arusha International Conference Centre (AICC). Balozi Taji ni Balozi Mstaafu wa Tanzania, Paris nchini Ufaransa

Teuzi hizi zimeanza tarehe 28 Desemba, 2021.

  • Amemteua Bw. Patience Kilanga Ntwina kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Bw. Ntwina alikuwa Mkurugenzi, Idara ya Katiba na ufuatiliaji wa Haki kutoka Wizara ya Katiba na Sheria.

Uteuzi huu umeanza tarehe 30 Desemba, 2021.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 31 Desemba, 2021 atalihutubia Taifa na kutoa Salamu za Mwaka Mpya 2022.

Katika hotuba yake hiyo, Mhe. Rais Samia anatarajia kutoa tathmini ya mwaka 2021 katika masuala mbalimbali yakiwemo masuala ya kiuchumi, kisiasa na kidiplomasia.

Pamoja na mambo mengine, Mhe. Rais Samia pia atatoa mwelekeo wa Serikali katika mwaka ujao wa 2022.

Hotuba hiyo inatarajiwa kurushwa mbashara saa 3:00 usiku kupitia vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mitandao ya kijamii ikiwemo YouTube chaneli rasmi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu ‘Ikulu Tanzania”.