Monthly Archives: April 2022

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Ashiriki katika Uzinduzi wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour Uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Arusha International Conference Centre AICC Jijini Arusha Tarehe 28 Aprili, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Arusha International Conference Centre AICC Jijini Arusha tarehe 28, Aprili, 2022.
 
Viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Arusha International Conference Centre AICC Jijini Arusha tarehe 28, Aprili, 2022.

 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwandishi wa Habari Maarufu wa Marekani ambaye ndiye mtayarishaji wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour Peter Greenberg mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mikutano wa Arusha International Conference Centre AICC Jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa Filamu hiyo tarehe 28, Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati akitoa misaada ya Vyakula mbalimbali pamoja na mafuta kwa vikundi 27 vya Watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi Mkoani Arusha tarehe 28, Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi mara baada ya kuwakabidhi msaada wa vyakula pamoja na mafuta kwa vituo mbalimbali 27 vya Watoto hao tarehe 28, Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya Heshima kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Eliya Mjatta kuthamini mchango wake katika Tasnia hiyo mara baada ya uzinduzi wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour Jijini Arusha 28, Aprili, 2022.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Awasili Mkoani Arusha mara baada ya Kuhitimisha Ziara yake ya Kikazi nchini Marekani Tarehe 28 Aprili, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati akitokea nchini Marekani tarehe 28 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Philip Isdor Mpango mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati akitokea nchini Marekani tarehe 28 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati akitokea nchini Marekani tarehe 28 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM -Bara Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati akitokea nchini Marekani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akielekea kuwasalimia Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha waliofika kumpokea wakati akitokea nchini Marekani tarehe 28 Aprili, 2022.
Kikundi cha ngoma za asili cha Kimasai kikitoa burudani mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tarehe 28 Aprili, 2022.
Viongozi mbalimbali, Wananchi wa Mkoa wa Arusha pamoja na Kilimanjaro wakisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa Ndege wa KIA tarehe 28 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akihutubia Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na Arusha mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa KIA wakati akitokea nchini Marekani tarehe 28 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiagana na Makamu wa Rais Mhe. Philip Isdor Mpango mara baada ya kuhutubia Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha tarehe 28 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa. Samia Suluhu Hassan akiagana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mara baada ya kuwahutubia Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na Arusha katika uwanja wa Ndege wa KIA.