Daily Archives: May 11, 2022

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan awasili Nchini Uganda kuanza Ziara ya Kikazi ya Siku Mbili Tarehe 10 Mei, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili Ikulu Entebbe nchini Uganda tarehe 10 Mei 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili Ikulu Entebbe nchini Uganda tarehe 10 Mei 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Museveni wakati akisalimiana na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Uganda mara baada ya kuwasili Ikulu Entebbe nchini Uganda tarehe 10 Mei 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Museveni wakati wa nyimbo za Taifa za Tanzania na Uganda zikipigwa katika mapokezi Rasmi kwenye Viwanja vya Ikulu vya Entebbe nchini Uganda tarehe 10 Mei 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Uganda kwa ajili yake mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Ikulu ya Entebbe nchini Uganda tarehe 10 Mei 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebbe nchini Uganda tarehe 10 Mei 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Museveni katika Ikulu ya Entebbe nchini Uganda tarehe 10 Mei 2022.
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan azungumza na Wanahabari katika Ziara yake ya Kiserikali Ikulu ya Entebbe nchini Uganda
.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS SAMIA ASHUHUDIA UTIAJI WA SAINI WA HATI YA USHIRIKIANO NCHINI UGANDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji saini wa Hati ya Ushirikano (MoU) mbili Ikulu Entebbe nchini Uganda.

Hati hizo ni pamoja na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa 400KV kutoka Masaka-Mutukula-Nyakanazi -Mwanza na nyingine ni kuhusu ushirikiano wa masuala ya Ulinzi na Usalama baina ya nchi hizo mbili.

Aidha, utiaji saini huo ulishuhudiwa pia na Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni ambapo amesisitiza kuendelea kushirikiana kwenye utenngenezaji wa chanjo na dawa za binadamu na mifugo.

Makubaliano pia ni kwamba Tanzania itaanza kununua dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI (ARVs) kutoka Uganda.

Miongoni mwa mengine yaliojadiliwa ni kufunguliwa upya kwa njia ya Mwanza – Port Bell Kampala, ambayo hapo awali ilikuwa haifanyi kazi lakini hivi sasa inafanya kazi.

Kwa sasa njia hiyo imepunguza kwa kiwango kikubwa muda wake wa mpito ambapo sasa huchukua siku 4 tu tofauti na siku 9 hapo awali, hivyo kupunguza gharama za kufanya biashara.

Wakati huo huo, Tanzania imekubali kupunguza gharama za usafirishaji ambapo kwa sasa Uganda italipa Dola za Kimarekani 10 kwa lori litakalopita kila kilomita 100 katika njia ya kutoka Mutukula hadi Dar es Salaam kuanzia mwaka mpya wa fedha Julai mosi mwaka huu.

Pia, Uganda imeahidi kutuma tani nyingine elfu 10 za sukari ili kufidia upungufu wa bidhaa hiyo Tanzania.