Daily Archives: May 12, 2022

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho kwa Naibu Makatibu Wakuu kama ifuatavyo:

  • Uteuzi:
  • Amemteua Dkt. Charles Enock Msonde kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI (Elimu). Bwana Msonde amechukua nafasi ya Bw. Gerald Mweli ambaye amehamishiwa Wizara ya Kilimo. Kabla ya uteuzi huu Dkt. Msonde alikuwa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).
  • Amemteua Dkt. Maduhu Kazi kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Dkt. Kazi amechukua nafasi ya Bwana Ramadhani Kailima aliyehamishiwa TAMISEMI. Kabla ya uteuzi huu Dkt. Kazi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC).
  • Uhamisho:
  • Bwana Ramadhan Kailima Kombweyi, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi amehamishwa na kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), amechukua nafasi ya Dkt. Switbert Zakaria Mkama ambaye amehamishiwa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano).
  • Bwana Gerald Mweli, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) amehamishwa na kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo.
  • Dkt. Switbert Zakaria Mkama, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) amehamishwa na kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, amechukua nafasi ya Bwana Edward Gerald Nyamanga ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Uteuzi na uhamisho huu umeanza tarehe 09 Mei, 2022.

Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Nishati ya Mafuta Uganda Tarehe 11 Mei, 2022


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Uganda mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mkutano kwa ajili ya kusikiliza majadiliano ya Wadau mbalimbali katika Sekta ya Uwekezaji wa Mafuta katika Jiji la Kampala nchini Uganda tarehe 11 Mei, 2022.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa akiwa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji pamoja na Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato wakiwa katika Kikao cha majadiliano ya Wadau mbalimbali katika Sekta ya Uwekezaji wa Mafuta katika Jiji la Kampala nchini Uganda tarehe 11 Mei, 2022.

Wadau kutoka Sekta mbalimbali nchini Tanzania wakiwa katika Kikao cha majadiliano ya Wadau kutoka Sekta ya Uwekezaji wa Mafuta katika Jiji la Kampala nchini Uganda tarehe 11 Mei, 2022.

Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato akizungumza katika Kikao cha majadiliano ya Wadau mbalimbali kwenye Sekta ya Uwekezaji wa Mafuta Jijini Kampala nchini Uganda tarehe 11 Mei, 2022.