Daily Archives: May 23, 2022

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  MHE. RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA YA KIKAZI NCHINI GHANA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anaondoka nchini leo kuelekea Accra, Ghana kwa ajili ya Ziara ya Kikazi ya siku tatu nchini humo.

Akiwa nchini Ghana, Mhe. Rais Samia anatarajia kushiriki Mdahalo wa Wakuu wa Nchi utakaojadili fursa zilizomo na changamoto zinazozikabili Nchi za Afrika ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabianchi, kupanda kwa bei ya vyakula na matumizi ya nishati endelevu.

Mhe. Rais Samia pia anatarajia kupokea Tuzo ya mwaka 2022 ya Babacar Ndiaye kwa mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji ambayo hutolewa kwa Mkuu wa Nchi iliyofanya vizuri zaidi.

Tuzo hiyo hutolewa kila mwaka katika Mkutano wa AfDB, ambao kwa mwaka 2022 unafanyika Accra, Ghana.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, Akutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya AngloGold Ashanti Tarehe 23 Mei, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya AngloGold Ashanti Dkt. Alberto Calderon mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 23 Mei, 2022.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika Picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya AngloGold Ashanti Dkt. Alberto Calderon mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 23 Mei, 2022.