Monthly Archives: July 2022

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UTEUZI NA MABADILIKO YA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa wapya 07 na kuwahamisha vituo vya kazi Makatibu Tawala wa Mikoa 10 na wengine 09 kubakia kwenye vituo vyao kama ifuatavyo:-

A)      MAKATIBU TAWALA WA MIKOA WAPYA

  1. Kamishna Dkt. Mussa Ali Mussa – Ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro.
  • Prof. Godius Walter Kahyarara – Ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita.  Alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara.
  • Mhandisi Leonard Robert Masanja – Ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Iringa.  Alikuwa Mkufunzi wa Chuo cha TANESCO Mkoani Dar es Salaam.
  • Toba Alnason Nguvila – Ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kagera.  Alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Mkoani Kagera.
  • Elikana Mayuganya Balandya – Ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza. Alikuwa Kamishna wa Bajeti Wizara ya Fedha na Mipango.
  • Prof. Siza Donald Tumbo – Ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga.  Alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo.
  • Dkt. John Rogath Mboya – Ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora.  Alikuwa Kamishna wa Idara ya Bajeti katika Wizara ya Fedha na Mipango.

B) WALIOHAMISHWA VITUO VYA KAZI:

  1. Missaile Albano Musa – Amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha. Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Songwe.
  • Rehema Seif Madenge – Amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam. Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Lindi.
  • Hassan Abbas Rugwa – Amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Katavi. Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam.
  • Ngusa Dismas Samike – Amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Lindi. Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza.
  • Msalika Robert Makungu – Amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mara. Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora.
  • Msovera Albert Gabriel – Amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma. Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mara.
  • Rodrick Lazaro Mpogolo – Amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya. Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Katavi.
  • Zuwena Omari Jiri – Amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Pwani. Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga.
  • Happiness William Seneda – Amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Songwe. Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Iringa.
  1. Rashid Kassim Mchata – Amehamishwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa. Alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma.

C) AMBAO WANAENDELEA NA VITUO VYA KAZI:

  1. Dkt. Fatuma Ramadhan Mganga – Anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma
  • Karolina Albert Mthapula – Anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Manyara.
  • Abdallah Mohamed Malela – Anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara.
  • Judica Haikale Omary – Anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Njombe.
  • Willy Lugahyulula Machumu – Anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro.
  • Steven Mashauri Ndaki – Anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma.
  • Dorothy Aidan Mwaluko – Anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Singida.
  • Prisca Joseph Kayombo – Anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu.
  • Pili Hassan Mnyema – Anaendelea kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Tanga.

Uapisho utafanyika Ikulu Chamwino, Dodoma tarehe 1, Agosti, 2022.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa Wapya 09, kuwahamisha vituo vya kazi Wakuu wa Mikoa 07 na wengine 10 kubakia kwenye vituo vyao kama ifuatavyo:

  1. WAKUU WA MIKOA WAPYA:
  1. Nurdin Hassan Babu – Ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido mkoani Arusha.
  • Fatma Abubakar Mwasa – Ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
  • Halima Omari Dendego – Ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
  • Dkt. Raphael Masunga Chegeni – Ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
  • Peter Joseph Serukamba – Ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
  • Kanali Ahmed Abbas Ahmed – Ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara. Alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani.
  • Kanali Laban Elias Thomas – Ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma. Alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.
  • Albert John Chalamila – Ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera
  • Dkt. Yahaya Esmail Nawanda – Ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu. Alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora mkoani Tabora.
  • WALIOHAMISHWA VITUO VYA KAZI:
  1. Anthony John Mtaka – Amehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
  • Queen Cuthbert Sendiga – Amehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
  • Waziri Waziri Kindamba – Amehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
  • Martin Reuben Shigella – Amehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
  • Omary Tebweta Mgumba – Amehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe.
  • Adam Kigoma Malima – Amehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
  • Rosemary Staki Senyamule – Amehamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita.
  • AMBAO WANAENDELEA NA VITUO VYA KAZI:
  1. Amos Gabriel Makalla – Anaendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
  • John Vianney Mongella – Anaendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
  • Mwanamvua Hoza Mrindoko – Anaendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
  • Charles Makongoro Nyerere – Anaendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
  • Zainab Rajab Telack – Anaendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
  • Juma Zuberi Homera – Anaendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
  • Thobias Emir Andengenye – Anaendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
  • Sophia Edward Mjema – Anaendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
  • Balozi Batilda Salha Burian – Anaendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
  1. Abubakar Mussa Kunenge – Anaendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Uapisho utafanyika Ikulu Chamwino, Dodoma tarehe 1, Agosti, 2022.