Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta wafungua Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) Jijini Arusha Tarehe 22 julai, 2022 Leave a reply Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Arusha waliohudhuria ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) uliofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta, Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni, Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye, pamoja na viongozi wengine wakivuta kitambaa kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) katika Sherehe zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta, Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni, Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye, pamoja na viongozi wengine wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) katika Sherehe zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta wakati wa Sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022. Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022. Kwaya ya Utumishi ikitoa burudani katika Sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022. . Muonekano wa Barabara ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) ambayo imefunguliwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta katika Sherehe zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022. .
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Ashiriki Mkutano wa 22 wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Jijini Arusha Tarehe 21 Julai, 2022 Leave a reply Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulionza tarehe 21 Julai, 2022 Jijini Arusha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha AICC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulionza tarehe 21 Julai, 2022 Jijini Arusha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha AICC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulionza tarehe 21 Julai, 2022 Jijini Arusha. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na baadhi ya Viongozi Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Wawakilishi wakati wa Wimbo wa Taifa wa Afrika Mashariki ukipigwa kwenye ukumbi wa Mikutano wa AICC Jijini Arusha kabla ya kuanza kwa Kikao cha Wakuu hao wa Nchi tarehe 21 Julai, 2022.