Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Awasili Nchini Senegal Tarehe 06 Julai, 2022 Leave a reply Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Leopold Sedar Senghor Jijini Dakar nchini Senegal tarehe 06 Julai 2022 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika zinazonufaika na Dirisha la Maendeleo ya Kimataifa (IDA Summit for Africa) . .
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan awapongeza Serengeti Girls Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Julai, 2022 Leave a reply Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa, Katibu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi, Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF Bw. Wallace Karia katika picha ya Pamoja na Timu ya Taifa ya Wanawake wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Gils) kabla ya hafla ya kuwapongeza iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Gils) pamoja na viongozi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo katika hafla aliyowaandalia wachezaji wa Timu hiyo kuwapongeza baada ya kufuzu kombe la Dunia la Vijana litakalofanyika nchini India. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa zawadi Nahodha wa Timu ya Taifa ya Wanawake wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Gils) Noela Luhala kwa niaba ya Wachezaji wenzake kwenye hafla ya kuwapongeza iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Julai, 2022.