Daily Archives: July 9, 2022

UTEUZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Kedmon Elisha Mapana kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Dkt. Mapana anachukua nafasi ya Bw. Godfrey Lebejo Mngereza ambaye amefariki dunia.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Mapana alikuwa Mhadhiri Mkuu, Idara ya Sanaa Bunifu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Uteuzi huu unaanza mara moja.

UTEUZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. Habibu Juma Saidi Suluo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA).

Bwana Suluo anachukua nafasi ya Bw. Gilliard W. Ngewe ambaye amemaliza Mkataba wake.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Suluo alikuwa Mkurugenzi wa Fedha na Uhasibu, Shirika la Wakala wa Meli za Tanzania. (TASAC).

Uteuzi huu unaanza mara moja.