Daily Archives: July 16, 2022

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ahutubia kwenye Kumbukizi ya Pili ya Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa, ZanzibarTarehe 14 Julai, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wageni waalikwa kwenye maadhimisho ya pili ya Kumbukizi ya Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa yaliyofanyika Katika Hoteli ya Golden Tulip Zanzibar tarehe 14 Julai, 2022
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais Mstaafu wa Msumbiji Joaquim Chissano mara baada ya kuhutubia katika maadhimisho ya pili ya Kumbukizi ya Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa tarehe 14 Julai, 2022.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya kumbukumbu na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais Mstaafu wa Msumbiji Joaquim Chissano pamoja na Wenza wa viongozi mara baada ya maadhimisho ya pili ya Kumbukizi ya Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa tarehe 14 Julai, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapa tuzo madaktari mara baada ya kuhutubia katika maadhimisho ya pili ya Kumbukizi ya Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa yaliyofanyika kwenye hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar tarehe 14 Julai, 2022.
.
Viongozi mbalimbali pamoja na Wageni Waalikwa wakiwa kwenye maadhimisho ya pili ya Kumbukizi ya Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa yaliyofanyika katika hotel ya Golden Tulip, Zanzibar tarehe 14 Julai, 2022.

Mhe. Rais Samia Ahutubia kwenye Maadhimisho ya Mkutano wa 20 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati (AMECEA) Jijini Dar es Salaam Tarehe 12 Julai, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Maaskofu kutoka nchi mbalimbali Barani Afrika pamoja na baadhi ya viongozi katika maadhimisho ya mkutano wa 20 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati (AMECEA) uliofanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere Convention Centre Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Julai, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsalimia Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Muadhama Kardinali Polycarp Pengo kwenye maadhimisho ya mkutano wa 20 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati (AMECEA) uliofanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere Convention Centre Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Julai, 2022.
 
Maaskofu wa Kanisa Katoliki kutoka nchi mbalimbali pamoja na Wageni wengine wakiwa kwenye maadhimisho ya mkutano wa 20 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati (AMECEA) uliofanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere Convention Centre Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Julai, 2022.
.