Daily Archives: July 25, 2022

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Akutana na Kuzungumza na Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye Ikulu Jijini Arusha Tarehe 23 Julai, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambae pia ni Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye alipowasili Ikulu ndogo ya Arusha tarehe 23 Julai, 2022.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambae pia ni Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye yaliyofanyika Ikulu ndogo ya Arusha tarehe 23 Julai, 2022.
 

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akutana na kuzungumza na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta pamoja na Viongozi wengine Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta mara baada ya kuhitimishwa kwa mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha AICC tarehe 22 Julai, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika AICC tarehe 22 Julai, 2022.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Somalia Mhe. Hassan Sheikh Mohamud mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha AICC tarehe 22 Julai, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Rais wa Somalia Mhe. Hassan Sheikh Mohamud mara baada ya kufungwa kwa mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha AICC tarehe 22 Julai, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Mwakilishi wa Rais wa Sudani Kusini ambaye ni Waziri wa Ofisi ya Rais ya nchi hiyo Dkt. Barnaba Maria Benjamin mara baada ya kufungwa kwa mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha AICC tarehe 22 Julai, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Rais wa Sudani Kusini ambaye ni Waziri wa Ofisi ya Rais ya nchi hiyo Dkt. Barnaba Maria Benjamin mara baada ya mazungumzo tarehe 22 Julai, 2022 Jijini Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Uchumi wa Afrika Dkt. Vera Songwe mara baada ya kufungwa kwa mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha AICC tarehe 22 Julai, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Uchumi wa Afrika Dkt. Vera Songwe mara baada ya mazungumzo yao tarehe 22 Julai, 2022 Jijini Arusha.