Daily Archives: August 1, 2022

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan awaapisha Wakuu wa Mikoa pamoja na Makatibu Tawala katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam Tarehe 01 Agosti, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Halima Omari Dendego kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Albert John Chalamila kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Agosti, 2022.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Agosti, 2022.
Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala walioapishwa pamoja na Viongozi wa Taasisi mbalimbali za Serikali wakila Kiapo cha Maadili kwa Viongozi katika hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Agosti, 2022.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Hamis Juma, Waziri wa TAMISEMI Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Kattanga, Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Daniel Chongolo kwenye picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa mara baada ya tukio la Uapisho, Ikulu Jijini Dar es Salam tarehe 01 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwaapisha Wakuu wa Mikoa pamoja na Makatibu Tawala kwenye hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Agosti, 2022.
 



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS SAMIA AZITAKA HALMASHAURI KUSIMAMIA MAPATO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi katika Halmashauri zote kuhakikisha kuwa fedha zinazotolewa na Serikali zinahudumia wananchi kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.assan 

Rais Samia amesema hayo katika hafla ya uapisho wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Aidha, Rais Samia amesema fedha hizo zitumike katika kusukuma miradi ya maendeleo ya wananchi ikiwemo elimu, maji na afya bila kubadilisha matumizi.

Rais Samia amewataka Madiwani na Makatibu Tawala katika Halmashauri kuacha tabia ya mvutano katika matumizi ya fedha za maendeleo kwa kuwa tabia hiyo inachelewesha ukamilikaji wa miradi.

Vile vile, Rais Samia amezitaka Halmashauri kupitia viwango vya ukusanyaji wa mapato na kuziba mianya ya upotevu wa mapato ili kuweza kujihudumia na kuweza kujikimu kwa mahitaji ya kiofisi.

Kwa upande mwingine, Rais Samia ameiagiza Ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha kuwa kila ngazi ya Viongozi wanaoteuliwa wanafanyiwa mafunzo ili kukumbushwa kuhusu uwajibikaji kwa wananchi na kulitumikia taifa ipasavyo.