Daily Archives: August 5, 2022

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS SAMIA AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI MBEYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Maji kuhakikisha huduma ya maji safi kwa wananchi katika miradi inayozinduliwa inakuwa endelevu.

Rais Samia amesema hayo leo wakati akizindua Mradi wa Maji wa Shongo – Mbalizi mkoani Mbeya uliogharimu shilingi bilioni 3.345.

Aidha, Rais Samia ameitaka Wizara hiyo kuhakikisha kuwa huduma ya maji safi inawafikia wananchi kwa uhakika kwa kuwa Serikali imetumia fedha nyingi kutekeleza miradi hiyo kwa manufaa ya wananchi.

Katika hatua nyingine, Rais Samia ameweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa jengo la afya ya huduma ya mama na mtoto hospitali ya Meta ambalo litakuwa na uwezo wa kuhudumia akina mama zaidi ya 300 litakapokamilika.

Ujenzi wa jengo hilo utakapokamilika litakuwa na uwezo wa kuhudumia kina mama wa mkoa huo na kutoka mikoa mingine ya Nyanda za juu Kusini.

Vile vile Rais Samia ameweka Jiwe la Msingi katika jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na kuwataka madiwani mkoani humo kuhakikisha kuwa asilimia 10 ya Halmashauri inatumika katika miradi ya maendeleo.

Rais Samia yuko mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi ya siku nne ambapo atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan aanza ziara Mkoani Mbeya kwa kuzungumza na Wananchi pamoja na kuzindua Miradi tarehe 05 Agosti, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali wakati akizindua Mradi wa Maji safi wa Mbalizi, Shongo-Igale katika eneo la Mbalizi Mkoani Mbeya leo tarehe 05 Agosti, 2022. Wengine katika picha ni Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungulia maji kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji safi wa Shongo-Mbalizi katika eneo la Mbalizi Mkoani Mbeya leo tarehe 05 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mbalizi mkoani Mbeya mara baada ya kuzindua mradi wa maji safi wa Shongo- Mbalizi tarehe 05 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi pamoja na Wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya Kitengo cha Wazazi na Watoto Wachanga Meta mara baada ya kuzindua ujenzi wa jengo la afya ya huduma ya mama na mtoto Meta Mkoani Mbeya tarehe 05 Agosti, 2022.
Jengo la afya ya Huduma ya Mama na Mtoto lililopo Meta Mkoani Mbeya ambalo limewekewa jiwe la Msingi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 05 Agosti, 2022.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mbeya waliofika kwenye hafla fupi ya uwekaji wa Jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mbeya zilizofanyika Jijini Mbeya tarehe 05 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisogeza kitambaa kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mbeya katika hafla fupi iliyofanyika Jijini Mbeya tarehe 05 Agosti, 2022.
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria hafla fupi ya uwekaji wa Jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mbeya katika hafla fupi iliyofanyika Jijini Mbeya tarehe 05 Agosti, 2022.