Daily Archives: August 6, 2022

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS SAMIA AFANYA ZIARA YA KIKAZI WILAYANI CHUNYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na TAMISEMI kupitia Halmashauri zote nchini na kuhakikisha zinaweka mipango ya kukusanya mapato.

Rais Samia amesema hayo katika hafla ya uzinduzi wa barabara ya Chunya -Makongolosi kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 39 iliyofanyika katika uwanja wa Matundasi.

Aidha, Rais Samia amesema mapato yanayokusanywa na Halmashauri yakisimamiwa vizuri yanaweza kujenga miradi ya maendeleo kwa ajili ya wananchi.

Akizungumza na wananchi wa Chunya mjini, Rais Samia ameagiza Madiwani na Wenyeviti wa eneo hilo wanaopata mapato mengi kutokana na kutoa leseni nyingi za biashara kujenga kituo cha mabasi cha Chunya.

Vile vile, Rais Samia ameeleza barabara hiyo itafungua fursa za kibiashara kwa wananchi wa Chunya kwani inaunganisha mkoa wa Mbeya na mikoa ya jirani.

Ziara ya Mhe. Samia Suluhu Hassan Wilaya ya Chunya tarehe 06 Agosti, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kuzungumza na Wananchi wa Kijiji cha Chalangwa Wilaya Chunya Mkoani Mbeya alipokua njiani akielekea Chunya mjini tarehe 06 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi wa Chunya Mjini Mkoani Mbeya alipokua njiani akielekea Makongorosi kwa ajili ya kukagua mradi wa Barabara ya kiwango cha lami km 39 Chunya Makongorosi tarehe 06 Agosti, 2022.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizinduzi mradi wa Maji Makongolosi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya tarehe 06 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisogeza kitambaa kuashiria uzinduzi wa mradi wa Maji Makongolosi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya tarehe 06 Agosti, 2022.
.
.
.
.
.
.
.
.