Daily Archives: August 7, 2022

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS SAMIA AFANYA ZIARA YA KIKAZI WILAYA RUNGWE NA KYELA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema mkoa wa Mbeya unakabiliwa na changamoto ya lishe bora kwa watoto licha ya kuwa mkoa huo unalima na kuzalisha chakula kwa wingi.

Rais Samia amesema hayo wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa John Mwakangale wilayani Kyela.

Aidha, Rais Samia amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kuhakikisha anatekeleza Mpango wa Pili Jumuishi wa Kitaifa wa Masuala ya Lishe (NMNAP II 2021 – 2026).

Vile vile, Rais Samia amewataka wananchi wa mkoa huo kuongeza jitihada katika masuala ya lishe bora ili kuimarisha afya za watoto.

Kwa upande mwingine, Rais Samia ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa kuwa na umoja na mshikamano na kufanya kazi kwa kushirikiana bila ya kujali itikadi zao. Rais Samia ameendelea na ziara yake mkoani Mbeya ambapo leo ametembelea Wilaya ya Rungwe na Kyela na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kuweka jiwe la msingi ujenzi wa kituo cha pamoja cha forodha mpakani mwa Tanzania na Malawi

Ziara ya Mhe. Rais Samia Wilaya ya Rungwe na Kyela Mkoani Mbeya tarehe 07 Agosti, 2022

.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi wa Tukuyu Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya tarehe 07 Agosti, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi wa Tukuyu Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya tarehe 07 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisogeza kitambaa kuashiria uzinduzi wa majengo mapya ya Chuo cha Ualimu Mpuguso Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya tarehe 07 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa majengo mapya ya Chuo cha Ualimu Mpuguso Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya tarehe 07 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisogeza kitambaa kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kituo cha pamoja cha Forodha Kasumulu Wilayani Kyela Mkoani Mbeya (mpakani ) na Malawi tarehe 07 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wananchi wa Kasumulu baada ya kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Kituo cha pamoja cha Forodha Kasumulu Wilayani Kyela Mkoani Mbeya tarehe 07 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Kikusya-Ipinda-Matema km 39 katika hafla fupi iliyofanyika Ipinda, Kyela Mkoani Mbeya tarehe 07 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Kikusya-Ipinda-Matema km 39 katika hafla fupi iliyofanyika Ipinda, Kyela Mkoani Mbeya tarehe 07 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi wa Tukuyu Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya tarehe 07 Agosti, 2022.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Kiwira wilayani Rungwe
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Ipinda, Kyela baada ya kufungua Barabara ya Kikusya-Ipinda-Matema km 39 katika hafla fupi iliyofanyika Ipinda, Kyela Mkoani Mbeya tarehe 07 Agosti, 2022.