Daily Archives: August 10, 2022
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RAIS SAMIA AWATAKA VIONGOZI KUWAHUDUMIA WANANCHI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imezuia kukata na kupandisha hadhi maeneo ya utawala kwa sababu yanaongeza gharama kwa Serikali.
Rais Samia amesema hayo leo wakati akihutubia wananchi wa Njombe katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba.
Aidha, Rais Samia amesema mwelekeo wa Serikali ni kunyanyua hali ya uchumi wa nchi ili kuinua hali ya maisha ya mwananchi mmoja mmoja.
Rais Samia pia ametoa wito kwa Viongozi nchini kusimamia ipasavyo miradi inayotekelezwa na Serikali ili kuwajengea fursa Watanzania kufanya shughuli za maendeleo na kuinua kipato. Vile vile, Rais Samia amewataka Viongozi wa Kata, Wilaya na Mikoa