Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ahitimisha ziara yake ya kikazi Mkoani Iringa Tarehe 13 Agosti, 2022 Leave a reply Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na kuagana na Viongozi pamoja na Wananchi wa Jimbo la Isimani Mkoani Iringa baada ya kukamilisha Ziara yake ya kikazi Mkoani humo tarehe 13 Agosti, 2022. . . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi na Wananchi wa Mkoa wa Dodoma alipowasili katika Kijiji cha Mpunguzi alipokuwa akitokea Mkoani Iringa baada ya kukamilisha Ziara yake ya kikazi tarehe 13 Agosti, 2022.
Ziara ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Mkoani Iringa tarehe 12 Agosti, 2022 Leave a reply Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kama ishara ya kuweka Jiwe la Msingi Mradi wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege Iringa. Hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi imefanyika katika Mtaa wa Mapanda kata ya Nduli Mkoani Iringa tarehe 12, Agosti, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mtaa wa Mapanda mara baada ya kuweka jiwe la Msingi Mradi wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa tarehe 12, Agosti, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Wananchi wa Mkoa wa Iringa alipowasili katika Uwanja wa CCM Samora kwa ajili ya kuhutubia Mkutano wa Hadhara tarehe 12 Agosti, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mkoa wa Iringa kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Uwanja wa CCM Samora tarehe 12 Agosti, 2022. . . . . .