Daily Archives: August 18, 2022

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan aanza ziara ya siku moja nchini Congo DRC tarehe 18 Agosti, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo wakipokea Gwaride rasmi alipowasili katika Viwanja vya Ikulu Jijini Kinshasa kwa ajili ya kuanza ziara rasmi ya siku moja nchini DRC tarehe 18 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo akikagua Gwaride rasmi alipowasili katika Viwanja vya Ikulu Jijini Kinshasa kwa ajili ya kuanza ziara rasmi ya siku moja nchini DRC tarehe 18 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo alipokua akitambulishwa kwa Viongozi mbalimbali wa DRC alipowasili katika Ikulu ya Kinshasa kwa ajili ya kuanza ziara rasmi ya siku moja tarehe 18 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo katika Ikulu ya Kinshasa nchini DRC tarehe 18 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo alipowasili katika Viwanja vya Ikulu ya Kinshasa tarehe 18 Agosti, 2022
 

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Ahudhuria Mkutano wa 42 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC nchini DRC Tarehe 17 Agosti, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo mara baada ya kuwasili katika Jiji la Kinshasa tarehe 16 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo mara baada ya kuwasili katika Jiji la Kinshasa tarehe 16 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo mara baada ya kuwasili Kinshasa nchini DRC tarehe 16 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo mara baada ya mazungumzo yao katika Jiji la Kinshasa tarehe 16 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa N’Dijili Kinshasa nchini DRC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 42 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika tarehe 17 Agosti, 2022 nchini humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Jean-Michel Sama Lukonde Kyenge mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa N’Dijili Kinshasa nchini DRC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 42 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika tarehe 17 Agosti, 2022 nchini humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Ujumbe wake wakiwa kwenye Mkutano wa 42 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika katika Mji wa Kinshasa nchini DRC tarehe 17 Agosti, 2022.
 


.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo Baada ya Mkutano wa Viongozi, Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika katika Mji wa Kinshasa nchini DRC tarehe 17 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitia saini moja ya maazimio katika Mkutano wa Viongozi, Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika katika Mji wa Kinshasa nchini DRC tarehe 17 Agosti, 2022.