Daily Archives: August 19, 2022

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Prof. Mark James Mwandosya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).  Prof. Mwandosya anachukua nafasi ya Prof. Jamidu Hazzam Yahaya ambaye amemalizia muda wake.

Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Agosti, 2022.