UTEUZI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua SACP Mzee Ramadhan Nyamka, Kaimu Kamishna wa Magereza Huduma za Urekebu kuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza.
SACP Ramadhan anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee ambaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Uteuzi wa SACP Mzee Ramadhan Nyamka umeanza tarehe 24, Agosti, 2022.