Daily Archives: August 26, 2022

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

  1. Amemteua Bw. Peter Ilomo kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF). Bw. Ilomo ni Katibu Mkuu Mstaafu. Bw. Ilomo anachuka nafasi ya Dkt. Moses M. Kusiluka ambaye amemaliza kipindi chake.
  • Amemteua Bi. Mwantumu Bakari Mahiza kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali. Bi. Mahiza ni Skauti Mkuu Tanzania.

Uteuzi huu unaanza mara moja

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akutana na Kuzungumza na Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Wakimbizi (UNHCR) Filippo Grandi, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 26 Agosti, 2022


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wakimbizi (UNHCR) Filippo Grandi mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 26 Agosti, 2022.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wakimbizi (UNHCR) Filippo Grandi mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 26 Agosti, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wakimbizi (UNHCR) Filippo Grandi mara baada ya mazungumzo yao, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 26 Agosti, 2022.