Daily Archives: September 5, 2022

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Asafiri kwa Meli kutoka Zanzibar kwenda Dar es salaam Tarehe 05 Septemba, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiingia ndani ya Meli ya Kilimanjaro 4 kutoka Bandari ya Malindi Zanzibar wakati alipokuwa akielekea Jijini Dar es Salaam  tarehe 05 Septemba, 2022
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania cMhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Abiria na Wananchi mbalimbali aliosafiri nao kwa Meli ya  M.V Kilimanjaro 4 alipokuwa akiondoka katika Bandari ya Malindi Zanzibar akielekea Jijini Dar es Salaam  tarehe 05 Septemba, 2022
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania cMhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Abiria na Wananchi mbalimbali aliosafiri nao kwa Meli ya  M.V Kilimanjaro 4 alipokuwa akiondoka katika Bandari ya Malindi Zanzibar akielekea Jijini Dar es Salaam  tarehe 05 Septemba, 2022
.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha kumbukumbu kwenye Meli ya Kilimanjaro 4 alipokuwa akiondoka katika Bandari ya Malindi Zanzibar akielekea Jijini Dar es Salaam  tarehe 05 Septemba, 2022
.
.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Ashiriki na Kuhutubia katika Tamasha la Kizimkazi, Zanzibar Tarehe 03 Septemba, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi mara baada ya kuwasili katika eneo la Kizimkazi Dimbani kwa ajili ya kushiriki kwenye Tamasha la Kizimkazi  tarehe 03 Septemba, 2022
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia bidhaa na vifaa vya matumizi ya aina mbalimbali katika mabanda ya Maonesho kwenye kilele cha   Tamasha hilo  la siku ya Kizimkazi tarehe 03 Septemba, 2022
.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kuhusu matumizi ya vifaa mbalimbali vya Uvuvi kutoka kwa Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo Zanzibar KMKM wakati alipotembelea mabanda ya Maonesho kwenye Tamasha la siku ya Kizimkazi tarehe 03 Septemba, 2022
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia Kiazi Kikuu kilichochimbuliwa kwenye ardhi kavu na Wazee wa Jadi kutoka Kikundi cha Shomoo cha Kizimkazi katika Siku ya kilele cha Tamasha hilo lililofanyika Kizimkazi Dimbani tarehe 03 Septemba, 2022
Wataalam wa Jadi wa Kikundi cha Shomoo cha Kizimkazi wakionesha uwezo wa kufanya vitu mbalimbali wakati wa Sherehe za Tamasha hilo lililofanyika Kizimkazi Dimbani, Zanzibar tarehe 03 Septemba, 2022.
.
.
.
Wasanii wa Kikundi cha Zanzibar One wakitoa burudani kwenye Tamasha hilo la Kizimkazi lililofanyika Kizimkazi Dimbani, Zanzibar tarehe 03 Septemba, 2022.
.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wageni mbalimbali wakati wa kilele cha Tamasha la Kizimkazi lillilofanyika Kizimkazi Dimbani tarehe 03 Septemba, 2022.