Daily Archives: September 9, 2022

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS SAMIA ATANGAZA SIKU TANO ZA MAOMBOLEZO YA KITAIFA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha Hayati Malkia wa Uingereza, Elizabeth II, kilichotokea tarehe 08 Septemba, 2022 nchini Uskochi

Maombolezo hayo yataanza tarehe 10 Septemba, 2022 hadi tarehe !4 Septemba, 2022.

Katika kipindi chote cha maombolezo, bendera zote zitapepea nusu mlingoti nchini Tanzania zikiwemo kwenye balozi zetu pia.

Rais Samia amewaomba Watanzania wote kuungana na wenzetu wa Uingereza katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na aliyekuwa kiongozi wao nchini humo.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan asaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia Kifo cha Malkia Elizabeth II wa Uingereza, Oysterbay Jijini Dar es Salaam Tarehe 09 Septemba, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia Kifo cha Malkia Elizabeth II (96) wa Uingereza aliyefariki tarehe 08 Septemba, 2022 nchini Uskochi. Mhe. Rais Samia alisaini Kitabu hicho katika Makazi ya Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Oysterbay Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Septemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania David Concar mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia Kifo cha Malkia Elizabeth II (96) wa Uingereza aliyefariki tarehe 08 Septemba, 2022 nchini Uskochi.
.