Daily Archives: September 12, 2022

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS SAMIA KUHUDHURIA HAFLA YA UAPISHO WA RAIS MTEULE WA KENYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuhudhuria hafla ya uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya  Mhe. William Samoei Ruto.

Aidha, Rais Samia atahudhuria uapisho huo wa Rais Ruto utakaofanyika jijini Nairobi kesho tarehe 13 Septemba, 2022.

Rais Samia ataambatana na baadhi ya Viongozi wa Serikali akiwemo Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara na Mhe. Harusi Said Suleiman, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ahutubia kwenye Kongamano la Wanawake na Vijana wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA), JNICC Jijini Dar es Salaam Tarehe 12 Septemba, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Viongozi mbalimbali wa Ndani na Nje ya Nchi kwenye Kongamano la Wanawake na Vijana wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) lililofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam tarehe 12 Septemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia Bidhaa katika mabanda mbalimbali ya Maonesho kabla ya kuhutubia viongozi mbalimbali wa Ndani na Nje ya Nchi kwenye Kongamano la Wanawake na Vijana wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) lililofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam tarehe 12 Septemba, 2022.
 
.
.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi kutoka nchi mbalimbali mara baada ya Kongamano la Wanawake na Vijana wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) lililofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam tarehe 12 Septemba, 2022.
.
.
.
.
.
.
.
.