Daily Archives: September 18, 2022

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

  1. Amemteua Prof. Mohamed Yakubi Janabi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili. Prof. Janabi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Prof. Janabi anachukua nafasi ya Prof. Lawrence Maseru ambaye amestaafu.

  • Amemteua Dkt. Peter R. Kisenge kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Dkt. Kisenge anachukua nafasi ya Prof. Janabi. Dkt. Kisenge ni Mkurugenzi wa Tafiti na Mafunzo wa (JKCI).

Uteuzi huu utaanza tarehe 02 Oktoba, 2022.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

  1. Amemteua Bw. Sosthenes Laurent Kewe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Tanzania (TIB). Bw. Kewe ni Mshauri Binafsi wa Uendelezaji wa Sekta Binafsi za Fedha, Dar es Salaam.
  • Amemteua Mhandisi Othman Sharif Khatib kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Bw Khatib anachukua nafasi ya Dkt. Jones Kilembe ambaye uteuzi wake umetenguliwa. Bw. Khatib ni Mhandisi Mstaafu (TCRA).
  • Amemteua Dkt. David Nkanda Manyanza kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI). Dkt. Manyanza ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Development Solution Consultancy (T) Limited.
  • Amemteua Bi. Hawa Abdulrahman Ghasia kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Masoko Kariakoo. Bi Ghasia ni Mbunge mstaafu.
  • Amemteua Bw. Sylvester Jospeh Kainda kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani. Bw. Kainda ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Morogoro.

Uteuzi huu unaanza mara moja.