Daily Archives: September 30, 2022

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS SAMIA AWAAGIZA WAKUU WA MIKOA KUSIMAMIA LISHE BORA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaagiza Wakuu wa Mikoa kuhakikisha fedha zilizopangwa kutekeleza mipango ya lishe zinatolewa kwa wakati.

Rais Samia ametoa agizo hilo leo wakati akihutubia Mkutano wa Mwaka wa Tathmini ya Sita ya Mkataba wa Lishe uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji, Mtumba.

Aidha, Rais Samia amesema kuwa mpango wa lishe mikoani hautekelezwi ipasavyo hivyo Wakuu wa Mikoa wanapaswa kujipanga na kuongeza jitihada za kuhamasisha utekelezaji wa shughuli za lishe bora na kuzipa kipaumbele ili zilete tija.

Kutokana na hilo, Rais Samia amemuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, kuwachukulia hatua stahiki Viongozi ambao wamefanya ubadhirifu wa fedha za lishe.

Rais Samia ameelekeza sekta zinazoguswa na utapiamlo ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda, afya na biashara kuweka mikakati ya kuhakikisha vyakula vinavyohitajika katika kukamilisha lishe vinapatikana na kuviongezea virutubisho hasa katika ngazi za chini.

Hali kadhalika, Rais Samia ameiagiza Wizara ya Afya kuifanyia mabadiliko Sera ya Taifa ya Lishe ya mwaka 1992 ambayo imepitwa na wakati ili iendane na hali halisi na mipango ya sasa hivi.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Azindua Chama cha Mawakili wa Serikali, Nembo ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Mfumo Rasmi wa Ofisi hiyo katika Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali Jijini Dodoma tarehe 29 Septemba, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na Mawakili wa Serikali kabla ya kuzindua Chama cha Mawakili wa Serikali, nembo na Mfumo rasmi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 29 Septemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitembelea mabanda mbalimbali likiwemo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kujionea shughuli mbalimbali pamoja na huduma zitolewazo na Ofisi hizo kabla ya kuhutubia na kuzindua Rasmi Chama cha Mawakili wa Serikali, nembo na Mfumo rasmi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kwenye laptop kuzindua mfumo rasmi wa Kieletroniki wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (OAGMIS), nembo  ya Ofisi hiyo pamoja na Chama cha Mawakili wa Serikali katika Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 29 Septemba, 2022.
Viongozi mbalimbali pamoja na Mawakili wa Serikali wakiwa kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma kwa ajili ya kushiriki Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali tarehe 29 Septemba, 2022.
.
.
.
.