Monthly Archives: October 2022

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Suzan Kaganda kuwa Kamishna wa Polisi.

Vile vile, Rais Samia amemteua Kamishna Kaganda kuwa Kamishna wa Utawala na Raslimali watu wa Jeshi la Polisi.

Kamishna Kaganda anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi (CP) Benedict Wakulyamba ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Uteuzi huu unaanza mara moja.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo wazungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam Tarehe 23 Oktoba, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Oktoba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo wakati wakishuhudia uwekaji saini Mkataba wa makubaliano baina ya Tanzania na DRC, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Oktoba, 2022. Kwa upande wa Tanzania, Mkataba huo ulisainiwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye na kwa upande wa DRC uliwekwa saini na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Christophe Lutundula.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Oktoba, 2022.